KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa matokeo waliyopata nyuma hawatayaangalia badala yake watapambana kupata pointi tatu mbele ya Fountain Gate.
Yanga Desemba 29 2024 inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa KMC na mchezouliopita walishinda ugenini Dodoma Jiji 0-4 Yanga.
Ni pointi 36 Yanga imekusanya baada ya mechi 14 ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ni mabingwa watetezi.
Kocha amesema: “Tumepata Muda mzuri wa kujiandaa na tayari tumewasoma Wapinzani wetu, Kiukweli ni Wapinzani Wagumu lakini kwa ukubwa wa timu hii pamoja na maandalizi yetu, tupo tayari kujitoa kwa asilimia mia moja ili kukusanya alama tatu”
“Kila Mchezo huja na Maandalizi tofauti, kwakuwa malengo yetu kesho ni kushinda basi tumejiandaa kucheza mchezo mzuri na kutengeneza nafasi za kutupa alama tatu.”
Kwa upanda wa nahodha Bakari Nondo ambeinisha kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao wataingia kwa tahadhari kupata matokeo mazuri.
“Tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa Leo, Sisi wachezaji tumejiandaa vizuri na mchezo wetu dhidi ya Fountain Gate, kilichobaki ni kusikiliza maelekezo ya Mwisho ya Mwalimu kwenye Uwanja wa Mazoezi Leo hii ili kuhahikisha tunatimiza Malengo yetu ya kupata alama tatu”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.