SIMBA YAITULIZA SINGIDA BLACK STARS KWA NGOMA

LICHA ya Simba kuvuna pointi tatu mbele ya Singida Black Stars kwa bao la Fabrice Ngoma dakika ya 42 ulikuwa ni mchezo wa mabavumabavu mwanzo mwisho.

Metacha Mnata kabla ya kufungwa alikuwa anapoteza zaidi ya sekunde 15 akiwa na mpira na baada ya Simba kufunga hali ikahamia kwa Mousa Camara.

Ni dakika 4 ziliongezwa kipindi cha kwanza na tatu kipindi cha piki huku mwamuzi Shomari Lawi akiwa pilato ambaye kuna namna mchezo ulionekana kuwa na kasi zaidi.

Pointi 40 Simba inafikisha baada ya mechi 15 inafunga 2024 ikiwa namba moja. Bao la Ngoma limetosha kuituliza Singida Black Stars inayonolewa na Ramadhan Nswanzurimo ambaye awali aliweka wazi kuwa mchezo utakuwa mgumu.

Mchezo wa pili Simba inashinda kwa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu ilitoka kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa KMC kwa bao la Jean Ahoua ambaye leo amekwama kumaliza dakika 90 baada ya kupata maumivu.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa ligi Yanga kete yao ni Desemba 29 itakuwa dhidi ya Fountain Gate Uwanja wa KMC Complex na Yanga kwenye msimamo ni yapili ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.