HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA BLACK STARS

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Singida Black Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.

Timu zote mbili ambazo zimekuwa kwenye mwendo mzuri zipo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa

Kwa upande wa kipa ni Mousa Camara, mabeki ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussen, Che Malone, Hamza.

Viungo ni Yusuph Kagoma, Fabrice Ngoma, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu, Kibu D.

Mshambuliaji ni Steven Mukwala ambaye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania alianzia benchi wakati ubao wa Uwanja wa KMC, Complex ukisoma Simba 1-0 JKT Tanzania kwa bao la Jean Ahoua pigo la penalti

Wachezaji wa akiba ni: Ally, Kijili Kelvin, Chamou, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Mavambo, Ateba, Awesu Awesu, Mashaka, Alexander.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.