KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC ni namba moja kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho.
Nyota huyo katoa pasi 9 msimu wa 2024/25 ambapo mbili alitoa kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania Desemba 27 2024 ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Azam FC 3-1 JKT Tanzania.
Pasi zote za mabao alimpa Idd Nado ambaye alifunga mabao mawili ilikuwa dakika ya 63 na 71 na bao la kuweka usawa kwa Azam FC lilifungwa na Pascal Msindo dakika ya 36.
Bao pekee kwa JKT Tanzania lilifungwa dakika ya 13 kwa pigo la faulo iliyopigwa na Said Ndemla ikamshinda mlinda mlango wa Azam FC katika harakati za kuokoa hatari hiyo ikazama nyavuni.
Ikumbukwe kwamba pasi ya kwanza msimu wa 2024/25 kwa Fei alimpa Nado kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC dakika ya 19 wamekuwa kwenye maelewano mazuri kwenye mechi ambazo wanacheza.
Azam FC inafikisha pointi 36 nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 16. Fei Toto kahusika kwenye mabao 13 yaliyofungwa na Azam FC kati ya 25 yaliyofungwa na timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.
Like
Comment
Send
Share