CLATOUS CHAMA MAMBO BADO YANGA

WAKATI mwamba Maxi Nzengeli akiwa chini ya uangalizi maalumu ndani ya Yanga bado kiungo Clatous Chama atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Fountain Gate.

Chama hakuwa kwenye mechi iliyopita dhidi ya Dodoma Jiji wakati ubao wa Jamhuri, Dodoma ukisoma Dodoma Jiji 0-4 Yanga mabao mawili ya Clement Mzize, Prince Dube alitupia bao moja na Aziz Ki bao moja kwa pigo la penalti.

Sababu kubwa ya Chama kutokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga anasumbuliwa na maumivu ya mkono ambapo alipata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Kiungo huyo ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC ni pasi mbili za mabao ametoa na kufunga bao moja msimu wa 2024/25.

Aliibuka ndani ya Yanga akitokea kikosi cha Simba baada ya mkataba wake kugota mwisho. Yanga ni nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na imekusanya pointi 36.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Fountain Gate, Desemba 29 2024 ikiwa ni mchezo wa funga Desemba 2024.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.