SINGIDA BLACK STARS YAIPIGA MKWARA SIMBA

UONGOZI wa Singida Black Stars umeweka wazi kuwa upo tayari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Desemba 28 2024 wanachohitaji ni pointi tatu muhimu.

Singida Black Stars baada ya kucheza mechi 15 imepata ushindi kwenye 10 ikiambulia sare katika mechi 3 na kupoteza ni mechi mbili pekee ndani ya msimu wa 2024/25.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 baada ya kukusanya pointi 33 ni moja ya timu ambazo zina safu kali ya ushambuliaji Bongo ambapo ni mabao 22 wamefunga kwenye mechi walizocheza ndani ya uwanja.

Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo na mpinzani wao anatambua kwamba mechi haitakuwa nyepesi hivyo wapo tayari.

“Hata Simba wanajua kwamba mchezo hautakuwa mwepesi maana nimemskia meneja wao wa Idara ya Habari akibainisha hivyo hilo lipo wazi tunawakaribisha nyumbani na kikubwa tunachohitaji ni matokeo mazuri.

“Unajua hata taarifa za wao kuja huku walikuwa wanaweka siri hapo unaona ni namna gani wanajua kwamba wanakutana na timu ya aina gani, tupo tayari na tunakwenda kufanya kweli kwenye mchezo wetu tukiwa nyumbani.”

Mkali wa kucheka na nyavu ndani ya NBC Premeir League ni Elvis Rupia ana mabao 8 yupo ndani ya Singida Black Stars.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.