YANGA YAIPIGIA HESABU DODOMA JIJI

 KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 za kazi.

Mchezo uliopita Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex ambapo Prince Dube alifunga bao moja, Clement Mzize alitupia bao moja huku Ibrahim Bacca akitupia mabao mawili.

Yanga mchezo wake ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji, unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma itakuwa ni Desemba 25 2024 kwa timu zote kupambania pointi tatu muhimu.

Ramovic amesema: “Nina wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, najivunia kwa hilo, lakini jambo muhimu kwa vijana hawa ni utimamu wa kimwili ili kukabiliana na wapinzani. Nataka kuona wachezaji wangu wote wakiwa na utimamu wa kimwili unaowiana.

“Hiyo itanifanya niwe na timu iliyokamalika. Mwanzo nilihitaji kuimarisha kwanza utimamu wa kimwili kwa kila mchezaji. Najua sio rahisi katika kipindi hiki kifupi ambacho nimekuwa hapa. Lakini nina furaha vijana wangu kuwa vijana wangu wote wana utayari wa kuwa na mabadiliko.”

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 3, Dodoma Jiji nafasi ya 11 ikiwa na pointi 16.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.