SIMBA V JKT TANZANIA TAMBO ZATAWALA

BAADA ya kutoka kuvuna pointi tatu mbele ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Desemba 21 na ubao kusoma Kagera Sugar 2-5 Simba leo watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania.

Simba inakutana na JKT Tanzania ambayo mchezo wao uliopita ilikuwa ugenini dhidi ya Namungo, baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-0 JKT Tanzania hivyo wakagawana pointi mojamoja.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu kutokana na aina ya timu wanayokwenda kukutana nayo lakini watajitahidi kufanya vizuri kuvuna pointi tatu.

“Ni mchezo mgumu tunajua lakini tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,unajua wapinzani wetu ni timu imara kutokana na mwendo ambao wanakwenda nao wachezaji nina amini watapambana kutimiza majukumu yao.”

Ahmad Ally, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa wanatambua mchezo wao utakuwa ni mgumu kutokana na kukutana na timu bora wataingia kwa tahadhari kupata matokeo mazuri.

“Tunakutana na timu bora ambayo imekuwa na matokeo mazuri hilo tunalitambua, maandalizi yapo vizuri hivyo tutaingia kwa tahadhari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.