AZAM FC KAZI IMEANZA HUKO

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwenye dirisha dogo la usajili itafanya usajili wa maana kutokana na mahitaji ya benchi la ufundi hivyo mashabiki wawe na subira kila kitu kipo kwenye mpango.

Azam FC kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 15 imekusanya pointi 33 ipo nafasi ya tatu vinara ni Simba wenye pointi 34 baada ya mechi 13 msimu wa 2024/25.

Katika sehemu ambazo zinatajwa kufanyiwa kazi na mabosi wa Azam FC ni eneo la ushambuliaji ambalo baada ya mechi 15 ni mabao 22 wamefunga.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kuna kila sababu za Azam FC kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kutokana na uwepo wa wachezaji wenye ubora ila watazingatia ripoti ya benchi la ufundi.

“Tupo vizuri na kwenye dirisha dogo la usajili tutafanya kazi kubwa kuongeza watu wa kazi kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi ni suala la muda kila kitu kitakuwa wazi mashabiki wawe na Subira muda upon a tutafanya jambo.”

Tayari Azam FC wametangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili kipa wao Zuber Foba ambaye atakuwa katika kikosi hicho mpaka 2027.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.