CAMARA Moussa ambaye ni jicho la timu amekuwa akifungwa mabao yanayotokana na kupunguza umakini hasa katika eneo lake.
Ukitazama mabao yote matano aliyofungwa ndani ya Ligi Kuu Bara amehusika kwa uzembe asilimia kubwa,Desemba 21 alikuwa shuhuda ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 2-5 Simba.
Mabao mawili dhidi ya Coastal Union, moja alifungwa akiwa ametoka katika eneo lake na bao moja ilikuwa kosa la viungo kupoteza mpira.
Mbele ya Yanga, pigo la faulo ya Clatous Chama hesabu zilimkataa katika kuokoa na mwisho mpira ukarudi ndani ya uwanja.
Mabao mawili dhidi ya Kagera Sugar kwa kipa anayecheza timu ya Simba hakupaswa kufungwa mabao yale, mabeki wanapaswa kuongeza umakini kwenye mawasiliano kutokana na safu hiyo kufanya makosa yanayofanana mara kwa mara.
Mwendelezo wa safu ya ulinzi ya Simba kufanya makosa bado umekuwa ni sababu ya kufungwa hivyo wote wanakazi kubwa kuwa imara hasa katika mechi zijazo.