MERIDIANBET YAENDELEA KUWEKEZA KWENYE MICHEZO

Katika harakati za kuhakikisha michezo inasonga mbele hasa mchezo wa mpira wa miguu wakali wa ODDS KUBWA Tanzania, Meridianbet leo hii wameamua kuwashika mkono timu ya mpira inayoitwa Jogoo Veteran ya Mbezi Juu.

Kampuni inayoongoza  katika sekta ya michezo na ubashiri Meridianbet,  imetoa msaada wa jezi mpya kwa timu ya mpira ya Mbezi Juu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia maendeleo ya michezo na kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za kijamii.

Timu hiyo ambayo imefikiwa na Meridianbet wakati huu ni Jogoo Veteran, ambayo ina wachezaji wazuri ambao wanashindana kwa hali na mali kufika zaidi ya hapo ambapo walipo na jezi hizo zitawasaidia kwenye majukumu yao ya kila siku kama kuzitumia wakiwa na mechi mbalimbali.

Vilevile leo hii una nafasi ya kuwa bingwa na Meridianbet  kwani odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Msafara huo wa Meridianbet ilikaribishwa na Diwani wa Mbezi Juu Mheshimiwa Anna Lukindo, ambaye alifurahi sana kuona ujio huo wa Meridianbet kwani wanasapoti wanamichezo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa jezi hizo, kukabidhi, Mhariri wa Meridianbet, Bi Nancy Ingram, alisema: “Tunajivunia sana kutoa msaada huu kwa Timu ya Jogoo Veteran, ambayo imekuwa nguzo muhimu katika kukuza michezo na umoja wa jamii hii. Tunategemea kwamba msaada wetu utaongeza nguvu kwa timu na kuhamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika michezo.”

Kwa upande wao, viongozi wa Timu ya Jogoo Veteran walishukuru Meridianbet kwa msaada wao, wakisema kwamba jezi mpya zitakuwa chachu ya kuongeza morali kwa wachezaji na kuhamasisha vipaji vipya miongoni mwa vijana.

Pia waliendelea kusema kuwa, “Huu ni msaada mkubwa kwetu, na tutahakikisha kwamba tunafanya mazoezi zaidi na kupambana kwa nguvu ili kuleta matokeo bora.”

Hii ni mojawapo ya juhudi za Meridianbet katika kuunga mkono maendeleo ya michezo na kukuza afya njema kwa jamii mbalimbali nchini Tanzania. Kampuni hiyo inaendelea kushirikiana na timu mbalimbali za michezo ili kuhakikisha kuwa michezo inakuwa sehemu ya maisha ya kila mtu.