MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Yanga Prince Dube aeweka rekodi yake ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick kwenye ligi akifungua akaunti yake ya mabao akiwa na uzi wa Yanga baada ya kusajiliwa na timu hiyo akitokea Azam FC.
Ipo wazi kwamba Dube ni mchezaji wa kwanza msimu wa 2024/25 kufunga hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa ni dhidi ya Mashujaa ya Kigoma, mwisho wa reli Desemba 19 2024.
Mabao hayo alifunga dakika ya 7 na dakika ya 21 kipindi cha kwanza Uwanja wa KMC, Complex na bao la tatu alifunga dakika ya 52 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-2 Mashujaa huku mabao ya Mashujaa yakifungwa na David Uromi dakika ya 45 na Idrisa Mohamed dakika ya 62.
Mshambuliaji huyo amesema kuwa ni furaha kwake kufunga ndani ya ligi kwa kuwa alikuwa anapitia kipindi kigumu jambo ambalo lilikuwa linampa presha kubwa.
“Nimefurahi kufunga na ninamshukuru Mungu, ilikuwa ni kipindi kigumu napitia lakini kwa sasa nimefunga nafurahi, nawashukuru mashabiki na wachezaji.Kuhusu kiatu cha ufungaji mimi sifikirii kwa kuwa kuna washambuliaji wengi wazuri na wanafunga.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.