MSHAMBULIAJI kiongozi kwenye safu ya ushambuliaji Leonel Ateba ni mabao matano amefunga kibindoni msimu wa 2024/25 akiwa amecheza mechi 9 na kukomba dakika 673.
Kwenye mechi mbili mfululizo Ateba amekuwa kwenye mwendelezo wa kufunga ndani ya ligi na kutwaa tuzo ya mchezaji bora mara baada ya dakika 90 kukamilika.
Ikumbukwe kwamba mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Leonel Ateba alifunga bao pekee la ushindi kwa pigo la penalti ubao ukasoma Pamba Jiji 0-1 Simba.
Mbele ya Ken Gold, Ateba alitupia mabao mawili yaliyoipa Simba pointi tatu, bao moja kwa pigo la penalti na moja kwa pigo la kichwa.
Mechi zote mbili alitwaa tuzo ya mchezaji bora. Amefikisha mabao matano na ana pasi moja ya bao kwa msimu wa 2024/25 ambapo Simba ni namba mbili kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 12.
Mshambuliaji huyo mara baada ya mchezo dhidi ya Ken Gold amesema kuwa ni furaha kwake kufunga kutokana na ushindani uliopo na anatambua kila mchezaji furaha yake ni kupata ushindi.
“Tumepata ushindi na nimefunga hii ni furaha kwangu na timu pia, tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi hivyo tupo imara na tutaendelea kupambana.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.