MSHAMBULIAJI wa Azam FC, mwili jumba, Alassane Diao amerejea kwa mara ya kwanza msimu wa 2024/25 uwanjani kwa kupata nafasi ya kucheza dhidi ya Fountain Gate ambapo aliingia kipindi cha pili akitokea benchi na kufunga bao moja kati ya mawili yaliyofungwa na timu hiyo.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Diao akiwa na uzi wa Azam FC kwa msimu mpya baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti ni dakika ya 80 aliingia akichukua nafasi ya Sillah katika mchezo huo.
Nyota huyo amesema ni furaha kubwa kurejea uwanjani na kufunga kwa kuwa inamuongezea hali ya kujiamini katika mechi zijazo.
“Nimefurahi kurejea na kufunga unajua kuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti ni jambo ambalo ni muhimu kwetu, tunaamini tutaedelea kupata matokeo kwenye mechi zijazo.”
Kwenye mchezo huo mabao ya Azam FC yalifungwa na Gibril Silla dakika ya 31 na Allasane Diao dakika ya 90 yalitosha kuituliza Fountain Gate.
Azam FC inafikisha pointi 33 ikiwa nafasi ya kwanza huku Fountain Gate ikiwa nafasi ya 6 na pointi zake kibindoni ni 20.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.