KATIKA mechi tano zilizopita ndani ya Ligi Kuu Bara Simba imefunga jumla ya mabao 10 kwa safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Leonel Ateba, Steven Mukwala wenye mabao mawilimawili, kinara kutoka Simba kwenye upande wa kutupia ni Jean Ahoua mwenye mabao matano na pasi nne za mabao.
Timu hiyo imekuwa na mwendelezo mzuri ndani ya ligi kwenye msako wa pointi tatu ambapo katika msako wa pointi 15 ilikomba zote ugenini na nyumbani iliposhuka kwenye dakika 90 za kusaka pointi tatu.
Mchezo uliopita ilikuwa dhidi ya Pamba Jiji baada ya dakika 90 ubao ulisoma Pamba Jiji 0-1 Simba, mechi nyingine ilikuwa Simba 4-0 KMC, Mashujaa 0-1 Simba, Simba 3-0 Namungo na Tanzania Prisons 0-1 Simba.
Katika mchezo dhidi ya Mashujaa wakiwa ugenini, Novemba Mosi 2024, Awesu Awesu alianzia benchi alipoingia alitoa pasi ya bao kwa Mukwala likiwa ni bao lake la pili kwenye ligi.
Desemba 18 2024 ni Simba v Ken Gold, Uwanja wa KMC, Complex ikumbukwe kwamba Ken Gold haijawa kwenye mwendo mzuri lakini imekuwa ikionyesha ushindani ndani ya uwanja.