YANGA WANA MATUMAINI YAKUTOSHA KIMATAIFA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa una matumaini makubwa kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye anga la kimataifa licha ya kuwa na pointi moja kibindoni.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic baada ya mechi tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika imegote kuvuna pointi moja baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya TP Mazembe.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kwa namna ambavyo wameanza kuwa na maelewano mazuri wachezaji na kasi waliyonayo wanaimani watafikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunakazi kubwa yakufanya kwenye mechi zetu mbili ambazo tutakuwa nyumbani kikubwa itakuwa kupambania pointi sita na mchezo wetu wa ugenini tutakuwa tunazihitaji pointi tatu hapo itakuwa kwenye mwendelezo wa kufuata malengo yetu ya kutinga hatua ya robo fainali.

“Pointi moja tuliyopata ugenini ina maana kubwa sana hivyo tunakwenda kupambana kusaka ushindi kwa kuwa tumerudi Dar ni maandalizi makini kwa mechi zetu zijazo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.