YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic imevuna pointi moja kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoshana nguvu kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa TP Mazembe ukisoma TP Mazembe 1-1 Yanga.
Katika mchezo wa Desemba 14 ambao ni watatu, Yanga ilianza kufungwa dakika ya 42 kupitia kwa Cheikh Fofana ambaye aliingia akitokea benchi kwenye mchezo wa leo dakika ya 32.
Bao hilo alimtungua Djigui Diarra ambaye alikwama kumaliza dakika 90 kwa kuwa hakuwa fiti na nafasi yake ilichukuliwa na Khomein.
Kipindi cha pili Yanga katika dakika za jioni ilipata bao la kuweka usawa kupitia kwa Prince Dube dakika ya 90 ikiwa ni bao la kwanza kwenye hatua ya makundi Yanga kufunga.
Pointi moja kibindoni baada ya mechi tatu ambazo ni dakika 270, wanarejea Bongo kwa maandalizi ya mechi zinazofuata kufungia Desemba 2024.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.