BAO la Prince Dube liliwapoteza TP Mazembe mazima kwa kuwa walikuwa wanaamini kazi imeisha lakini jioni wakatunguliwa bao moja na kugawana pointi mojamoja na Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Faida ya kutumia washambuliaji wawili imekuwa na faida unaona ni Clement Mzize alikuwa eneo la tukio akafanya jaribio kuelekea langoni na kipa akatema unakutana na Dube ambaye alikuwa eneo la tukio.
Pointi moja ugenini katika hatua ya makundi si haba wamerejea Dar kwa mechi zinazofuata ambapo mbili ni nyumbani kazi kwao kupata pointi tatu mazima katika mechi mbili sio kazi nyepesi.
Kundi A, Al Hilal amekuwa mwiba kwenye mechi tatu alizocheza zote kashinda akiwa kakusanya pointi 9 kibindoni ni namba moja anafuatiwa na MC Alger mwenye pointi nne, TP Mazembe nafasi ya tatu na pointi mbili huku Yanga nafasi ya nne na pointi moja.
Al Hilal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MC Alger kupitia kwa bao la Guessouma Fofana alifunga bao hilo dakika ya 76 likadumu mpaka mwisho wa mchezo huku TP Mazembe 1-1 Yanga, bao la TP Mazembe lilifungwa na Cheikh Fofana ilikuwa dakika ya 42.
Mechi zijazo kwa kundi A itakuwa ni Yanga v TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa na Al Hilal v MC Alger ambapo kwa Yanga kuendelea kufufua matumaini kutinga hatua ya robo fainali ni lazima ashinde hapo kisha matokeo ya mechi nyingine yataamua atakuwa nafasi ipi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.