TABORA UNITED ‘YAWAKANDA’ AZAM NYUMBANI BAO 2-1

Tabora United haijapoteza mchezo wowote kwenye mechi sita zilizopita kwenye Ligi Kuu bara wakishinda 5 na kutoka sare mchezo mmoja licha ya kukutana na wababe kama Yanga Sc, Azam Fc na Singida Black Stars mpaka sasa.

Kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam Fc, Tabora United imefikisha pointi 24 baada ya mechi 14 na wanasalia nafasi ya 5 huku Wanalambalamba ambao wanaendelea kusalia kileleni wakisalia na pointi 30 baada ya mechi 14.

FT: Tabora United 2-1 Azam Fc
⚽ 37’ Makambo
⚽ 68’ Makambo
⚽ 70’ Diaby

Tabora kwenye michezo 6 iliyopita
:
✅ Tabora Utd 1-0 Pamba Jiji
✅ Tabora Utd 1-0 Mashujaa
✅ Yanga Sc 1-3 Tabora Utd
🤝 Tabora Utd 2-2 Singida Black Stars
✅ Kmc Fc 0-2 Tabora Utd
✅ Tabora Utd 2-1 Azam Fc