HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA TP MAZEMBE

WAWAKILISHI wa Tanzania, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic leo wana kazi kusaka pointi tatu ugenini dhidi ya TP Mazembe mchezo wa hatua ya makundi.Hili hapa jeshi la Yanga ambalo litaanza ugenini kwenye mchezo wa tatu kimataifa: Diarra, Dickson Job, Bacca, Maxi Nzengeli, Khalid Aucho, Kouassi Yao, Kennedy Musonda, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya, Nickson Kibabage, Duke Abuya.
Katika wachezaji wa akiba ni Khomeiny, Nondo, Aziz Ki, Kibwana Shomary, Clatous Chama, Sure Boy, Jonas Mkude, Mzize, Dube.

Ipo wazi kuwa kwenye mechi mbili zilizopita moja Uwanja wa Mkapa na moja ugenini Yanga ilikwama kupata pointi tatu hivyo leo ina kibarua cha kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kusepa na pointi tatu licha ya kwamba mchezo hautakuwa rahisi.

Ramovic Sead, Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kwamba anatambua ugumu wa wapinzani wao TP Mazembe watapambana kupata matokeo mazuri ugenini.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.