HAO TABORA UNITED WANA BALAA ZITO, SIO YANGA, AZAM KICHAPO

TABORA United inayonolewa na Kocha Mkuu, Anicet Kiazmak imekuwa katika mwendo bora kwenye msako wa pointi tatu ndani ya NBC Premier League ikiwapa tabu washindani wake ndani ya dakika 90.

Katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa Desemba 13 2024 walisepa na pointi tatu mazima dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 2- 1 Azam FC. Katika mechi sita zilizopita waliambulia sare moja pekee ilikuwa dhidi ya Singida Black Stars walipotoshana kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Mechi nyingine ilikuwa ni ushindi kwa Tabora United namna hii: Tabora United 1-0 Pamba Jiji, Tabora United 1-0 Mashujaa, Yanga 1-3 Mashujaa, KMC 0-2 Tabora United.

Kutokana na ushindani kuwa mkubwa, Tabora United wameonekana kuwa na balaa zito kwa kuwa sio Yanga wala Azam FC wao wametembeza vichapo kwa timu hizo ambazo zipo ndani ya tatu bora.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.