YANGA KWENYE PRESHA KISA KUPOTEZA, KAZINI KIMATAIFA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic ameweka wazi kuwa wapo kwenye presha kubwa kwa sasa kwenye mechi za kimataifa kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal lakini watapambana kupata matokeo mazuri.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza kwa Yanga katika hatua ya makundi walikuwa nyumbani na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 0-2 Al Hilal, leo Desemba 7 wanakibarua ugenini Uwanja wa 5 July 1962 kusaka ushindi dhidi ya MC Alger, Waarabu wa Algeria.

Kocha huyo amesema kuwa licha ya kukutana na timu yenye upinzani mkubwa na kocha mwenye uzoefu wapo tayari kwa ajili ya kupambana kuwapa furaha mashabiki kwa kupata matokeo mazuri.

 “Tuko kwenye presha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, lakini imetupa nguvu ya kujiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu ujao. Tumekuja mapema kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa. Hatuwezi kupanga matokeo ya mwisho yatakavyokuwa lakini tunaweza kupanga jinsi tutakavyocheza ili kupata matokeo mazuri.

“Sio nzuri kucheza mechi bila mashabiki, binafsi napenda kuiona timu yangu ikicheza mbele ya mashabiki wengi, lakini tutawakosa mashabiki hapa uwanjani hivyo tuna jukumu la kupambana kuwapa furaha mashabiki wetu watakaokuwa nyumbani.

“Yanga wana historia kwenye uwanja tutakaotumia, walipoteza mchezo wa fainali hapa kwa kanuni lakini naamini walishinda mioyo ya wapenda mpira hapa Algeria, itakuwa ni siku nyingine na tutakuja na nguvu nyingine ya kutaka kushinda mchezo.

“Tunakwenda kucheza na timu ngumu, ina wachezaji bora na kocha mzoefu lakini upande wetu tuna kikosi chenye wachezaji bora sana, naamini itakuwa mechi nzuri yenye kuvutia.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.