MWANDISHI mkongwe na maarufu wa michezo nchini, Saleh Ally maarufu kama Saleh Jembe, kwa mara nyingine tena ameandika rekodi nyingine chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Fifa imemteua Saleh Jembe kwa mara ya tano mfululizo kupiga kura ya Mchezaji Bora wa Dunia ikiwa ni rekodi kubwa kuandikwa kwenye historia ya soka.
Fifa huchagua waandishi kutoka kila nchi na huangalia vigezo mbalimbali likiwemo suala la uzoefu, kuaminika, wingi wa kazi alizofanya mhusika kimataifa na hasa katika michuano na ligi kubwa.
Saleh jembe ndiye mwandishi mwenye mahojiano na makala nyingi zaidi za ana kwa ana kimataifa katika michezo na hasa soka na nyingi akiwa amefanya katika Klabu za EPL, Bundesliga na La Liga kama Real Madrid, Barcelona, Everton, Man United, Borussia Dortmund na nyingine nyingi.