YANGA HAO KAMILI KUWAKABILI WAARABU KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika leo wanatarajiwa kuwasili Algeria kwa maandalizi ya mwisho wa mchezo wao dhid ya MC Alger unaotarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024.

Msafara wa Yanga ulikwea pipa Bongo mapema Desemba 3 na walifika Dubai ambapo walipumzika.

Miongoni mwa wachezaji waliopo katika msafara wa Yanga ni Khalid Aucho, Clement Mzize, Jean Baleke, Prince Dube, Kennedy Musonda.

Ikumbukwe kwamba Aucho, Mzize hawa walikosekana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal uliochezwa Uwanja wa Mkapa na mwisho ubao ukasoma Yanga 0-2 Al Hilal.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo ujao ni mgumu na wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

“Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na wachezaji wapo sawa hivyo mashabiki waliopo Tanzania waendelee kutuombea na tunaamini tutapata matokeo mazuri.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.