KATIKA chati ya wakali wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara namba moja katika NBC Premier League ni Seleman Mwalimu kutoka Fountain Gate iliyofungua pazia la ligi kwa kucheza dhidi ya Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Mwalimu ambaye ni mzawa katupia mabao 6 kibindoni anafuatiwa na Jean Ahoua wa Simba mwenye mabao matano na pasi nne za mabao.
Elvis Rupia wa Singida Black Stars ni mabao matano katupia akitupia matatu kwa mapigo ya vichwa mwendo wa waaa.
Edger William kutoka Fountain Gate katupia mabao manne ndani ya kikosi hicho ambacho kimekuwa kwenye mwendo wake msimu wa 2024/25 katika kusaka ushindi yupo sawa na Yacouba Sogne wa Tabora United kamfikia naye ametupia mabao manne.
Peter Lwasa wa Kagera Sugar, Nassoro Saadun wa Azam FC, Paul Peter wa Dodoma Jiji, Offen Chikola wa Tabora United na Feisal Salum wa Azam FC wote wametupia mabao mannemanne.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.