YANGA WANAZIDI KUIMARIKA

BAADA ya kukiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 kocha mpya wa timu hiyo amebainisha kuwa wanazidi kuimarika taratibu kutokana na mwendo wa timu hiyo ndani ya uwanja.

Mchezo wa kwanza kwa kocha huyo ilikuwa dhidi ya Al Hilal ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-2 Al Hilal uliopewa jina la Dube Day ambapo mwisho walipoteza pointi tatu nyumbani na mchezo wa pili ulikuwa ni wa ligi walikomba pointi tatu ugenini.

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic ameweka wazi kuwa wanazidi kuimarika kutokana na mwendelezo wa mazoezi ambayo wanafanya huku ushirikiano ukizidi kuwa mkubwa.

“Tuna kazi kubwa yakufanya kwenye mechi zetu, ushirikiano unazidi kudumu na kila mchezaji anaonyesha uwezo wake hivyo nina amini bado tunazidi kuimarika na tutakuwa na matokeo mazuri. Ushindi unatupa nguvu ya kujiamini zaidi na makosa ambayo yamepita tunayafanyia kazi.”

Mchezo ujao kwa Yanga utakuwa wa kimataifa kwenye hatua za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024 Yanga inatarajiwa kuwa na kibarua dhidi ya MC Alger ugenini.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.