KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kipo kwenye maandalizi ya mechi za kimataifa ambapo mazoezi wanafanyia Mo Simba Arena kabla ya kukwea pipa kuwafuata wapinzani wao nchini Algeria. Kwenye uwanja wa mazoezi wamekuwa wakipewa mbinu mbalimbali kuwa fiti wachezaji.