KUMBILAMOTO CUP HAWA HAPA KUKIWASHA FAINALI

WANAUME 22 wanatarajiwa kuwa kwenye kazi msako wa mshindi wa taji la Kumbilamoto Cup 2024 kwenye fainali inayosubiriwa kwa shauku kubwa.

Mashindano hayo yenye ushindani mkubwa yalianza kutimua vumbi Septemba 16 2024 na mchezo wa ufunguzi uliwakutanisha wababe wawili ambao ni Watasu FC ilikuwa dhidi ya Bodaboda na wote hawajafika katika hatua ya fainali.

Desemba 2 2024 ilipigwa moja ya mechi kali iliyokuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Msikate Tamaa kati ya  Saigon FC  dhidi ya Stoke City FC.

Mbabe wa mchezo huo ni Saigon FC ambaye aliibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa nusu fainali na kutinga hatua ya fainali ya Kumbilamoto Cup kwa ushindi dhidi ya Stoke City FC kwa bao 1-0.

Fainali ya mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kumbilamoto Foundation, Tandika Plaza inatarajia kuchezwa Desemba 7, 2024 Uwanja wa Msikate Tamaa Vingunguti kati ya Bajaji FC dhidi Saigon FC na Desemba 6 utapigwa mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.