HUYU HAPA MKALI WA MABAO YA VICHWA

WAKATI wa usajili kwa msimu wa 2024/25 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally aliweka wazi kuwa kuna staraika refu kuliko goli ambalo lenyewe haliruki mipira ya juu bali ni waa, mpira upo kambani.

Nyota huyo ni Steven Mukwala ambaye kafunga jumla ya mabao mawili kwenye ligi na katika mabao hayo kafunga moja kwa pigo la kichwa ilikuwa dhidi ya Mashujaa mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Kuna mwamba yupo Singida Black Stars anaitwa Elvis Rupia yeye ni mkali wa mabao ya kichwa halafu haruki sana ni kukaa kwenye nafasi kisha Waa ngoma ipo kambani akiwaliza makipa kwenye mechi za ushindani.

Rekodi zinaonyesha kuwa Rupia katupia jumla ya mabao matano ndani ya ligi akiwa miongoni mwa nyota wenye mabao mengi kinara ni Suleiman Mwalimu huyu yupo ndani ya kikosi cha Fountain Gate.

Katika mabao hayo matano aliyofunga ni mabao matatu katupia kwa mapigo ya vichwa na mabao mawili kafunga kwa mguu wa kulia.

Timu ambazo amezifunga ni Ken Gold na Azam FC kwa mapigo ya mguu wa kulia huku Ken Gold, KMC na Tabora United ilikuwa mwendo wa Header.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.