DUKE Abuya, nyota wa mchezo mbele ya Namungo ameweka wazi kuwa wanaamini wataendelea kushinda mechi zijazo za ushindani.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa funga kazi Novemba kwa Yanga ilikuwa dhidi ya Namungo, Novemba 30 2024 baada ya dakika 90 ubao ukasoma Namungo 0-2 Yanga.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Sead Ramovic mrithi wa mikoba ya Miguel Gamondi ambaye alikutana na Thank You ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi.
Pointi hizo tatu zimeipeleka Yanga nafasi ya tatu na pointi 27 kibindoni tofauti ya pointi moja na vinara wa ligi ambao ni Simba wenye pointi 28 wote wakiwa wamecheza mechi 11.
Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Kennedy Musonda, Pacome Zouzoua yakitosha kuipa pointi tatu Yanga huku Duke akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Kiungo huyo amesema: “Tunamshukuru Mungu kwa ushindi na mashabiki kujitokeza kwa wingi, tunaamini kwamba tutaendelea kushinda mechi zijazo.”
Mchezo ujao kwa Yanga utwakuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger unatarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024 ambapo wawakilishi hawa wa Tanzania kimataifa watakuwa ugenini.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.