MSTAHIKI Meya wa Dar, Omary Kumbilamoto ambaye ni diwani wa Kata ya Vingunguti, amekabidhi vifaa vya michezo kwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo Gongolamboto.
Kumbilamoto ametimiza ahadi hiyo baada ya kuombwa na wanafunzi wa shule hiyo wakati alipoalikwa katika mahafali yao hivyo ametimiza jambo hilo kwa ajili ya kuibua vipaji kwa wachezaji ambao wapo shuleni.
Ikumbukwe kwamba huu ni utekekezaji wa maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kusapoti michezo mashuleni.
Kumbilamoto ni mwanafamilia ya michezo ambapo kwa sasa kuna mashindano makubwa yanayoendelea kata ya Vingunguti yanakwenda kwa jina la Kumbilamoto Cup ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa sasa.
Kwenye mashindano hayo Kumbilamoto alitoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki ikiwa ni jezi na mipira ambapo ushindani umekuwa mkubwa kila iitwapo leo.
“Mama anatekeleza kwenye kila sekta na anapenda kuona michezo ikiimarika kuanzia ngazi ya chini, tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na malengo yetu ni kuona kila idara inafanya vizuri ikiwa ni pamoja na sekta ya michezo ambapo anahitaji kuona tunasapoti michezo mashuleni.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.