HIZI HAPA DAKIKA 450 FUNGA KAZI UNYAMANI 2024

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika wanakete tano za kazi kufungwa mwaka 2p24 katika mechi za ushindani.

Mechi tano za nguvu ambazo ni dakika 450 kwenye msako wa pointi tatu na kumbuka kwamba watakutana na mbabe wa Yanga, Tabora United kwenye mchezo wa mwisho wakiwa ugenini.

Rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya 2024/25 Tabora United ni timu ya kwanza kufunga mabao zaidi ya mawili mbele ya mabingwa watetezi Yanga ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma, Yanga 1-3 Tabora United.

Ipo wazi kwamba mchezo wa kufunga Novemba ilikuwa katika kombe la Shirikisho Afrika walipopata ushindi wa bao 1-0 Bravos, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Novemba 27 2024.

Desemba 8 2024 watakuwa kimataifa dhidi ya CS Constantine ugenini, Desemba 15 itakuwa Simba v Sfaxine kimataifa Uwanja wa Mkapa.

Desemba 18 itakuwa dhidi ya Ken Gold, NBC Premier League Uwanja wa KMC, Desemba 21 itakuwa dhidi ya Kagera Sugar ugenini na funga kazi itakuwa ugenini dhidi ta Tabora United.

Mchezo dhidi ya Tabora United unatarajiwa kuchezwa Desemba 28 2024 Simba itakuwa ugenini ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.