>

SIMBA YAIVUTIA KASI AL HILAL KIMATAIFA

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa maandalizi ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal yamekamilika kwa asilimia kubwa na kilichopo kwa sasa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa wachezaji ambao walikuwa wamepewa mapumziko baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Fountain Gate wanarejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo huo rasmi.

“Kikosi kinarejea kambini rasmi Agosti 28 2024 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan kila mmoja anaifahamu maarufu kama timu ya Ibenge ambapo mchezo huo utachezwa saa 10: 00 jioni huu ni uwanja wetu wa nyumbani na tutacheza hapo pia.

“Viingilio kwenye mchezo wetu huu wa kimataifa ni 10,000 kwa mzunguko na 20,000 VIP hii ni kutokana na hadhi ya mchezo wetu na hadhi ya mpinzani wetu tayari kila kitu kimekamilika na Al Hilal ya Sudan wapo tayari nchini.

Ni Jumamosi ya funga Agosti mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa kwa timu hizo mbili kupimana uwezo katika anga la kimataifa Uwanja wa KMC, Mwenge.