>

KAGERA SUGAR FC DHIDI YA YANGA KUPIGWA KESHO SAA 11:00 JIONI

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya muda kwa michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC ambapo mchezo wa Kagera Sugar FC dhidi ya Yanga ambao ni mchezo namba 8, sasa utafanyika Agosti 29, 2024, saa 11:00 jioni badala ya saa 12:30 jioni kama ilivyopangwa awali.

Kwa mchezo namba tatu kati ya Namungo FC na Fountain Gate FC ambao ulipangwa kuchezwa Agosti 29, 2024 katika Uwanja wa Majaliwa, Lindi, umebadilishwa muda na sasa utafanyika saa 1:30 usiku badala ya saa 2:30 usiku.

Kwa mujibu wa TPLB, mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia mapendekezo kutoka kwa wadhamini wenye haki ya kurusha matangazo ya televisheni, ili kuruhusu urushaji bora wa michezo hiyo.