>

TANO KUNTU ZA HANS RAFAEL MECHI YA SIMBA DHIDI YA FOUNTAIN GATE

1. SIMBA WANACHEZA KWA MALENGO

Yes! Mnyama anashinda kwa swagger,mnyama anapika kila kiumbe mbele yake,magoli ya kideo yanafungwa na cleen sheet zinapatikana…mechi mbili goli (7) na Cleen sheet (2),mnyama kileleni anapepea

2. DEBORAH FERNANDEZ ROLE

Kuna namna Fadlu anamtumia Fernandez kwenye kikosi chake,wakati Simba wanatoka nyuma Kapombe anapewa uhuru mkubwa wa kupanda mbele kisha Debora anashuka kwenye nafasi ya Kapombe na kutengeneza Back 3 ya uongo……ni wazi Fadlu anahitaji Assist nyingi kutoka kwa Shomari.

3. FADLU AMEMPUNGUZIA MAJUKUMU AHOUA

Jean ni dynamic presser,Jean ni assister,Jean ni goal scorer hivyo hutakiwiki kumpa mzigo mkubwa wa kukimbia eneo kubwa la uwanja,Ahoua anatakiwa kukupa magoli na assist….baada ya Fadlu kugundua hilo amemkatia kipande cha kuzunguka ambacho ni kuanzia Zone ya 11 hadi Zone ya 17 kisha Awesu alitakiwa kushuka kwenye Zone ya 8 kuungana na Mzamiru ili kudumisha “overload” wakati Simba wanatoka nyuma.

4. BALUA ANAITAKA NAMBA YA KIBU

Kila mtu anaruhusiwa kuishi maisha mazuri na hivi sasa Edwin Balua anaishi maisha ya ndoto zake,kijana ana kasi,anafunga magoli ya kila aina kuanzia mguuni,kichwani na mipira ya kutengwa….Kibu ana kazi ya ziada kurejesha nafasi yake

5. FOUNTAIN GATE WAJIANGALIE

Sielewi huko mbeleni itakuaje ila Fountain Gate wajiangalie sana maana msimu huu ushindani ni mkubwa sana…..Mimi binafsi Sijaona utashi,muunganiko na quality ya kikosi chao.

NB:Kwenye mechi zenu mbili mnatakiwa kushinda magoli zaidi ya 7 ili kumshusha mnyama kileleni