>

AZAM FC MATAJIRI WA DAR KIMATAIFA MWENDO WAMEUMALIZA

MATAJIRI wa Dar, Azam FC kwenye anga la kimataifa mwendo wameuliza kwa kufungashiwa virago na APR ya Rwanda katika hatua a awali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar Azam FC inyonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph  Dabo ilipata ushindi wa bao 1-0 hivyo ilikuwa na kibarua cha kulinda ushindi huo na kuongeza mabao mengi jambo ambalo halikufanikiwa kwenye mchezo wa pili.

Katika mchezo wa pili uliochezwa nchini Rwanda baada ya dakika 90 ubao ulisoma APR 2-0 Azam FC hivyo APR wamepindua meza kibabe na kusonga hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1.

Azam FC imerejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara ambayo imeanza Agosti 16 na mchezo wa kwanza wa ufunguzi ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba baada ya dakika 90 ubao ulisoma Pamba Jiji 0-0 Tanzania Prisons.

Mwandishi wa Habari za Michezo Bongo mwenye uzoefu kwa muda mrefu akiishi maisha ya mpira Saleh Ally, wengi hupenda kumuita Jembe ameweka wazi kuwa sio jambo la kufurahisha kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuishia hatua ya awali hasa washindi wa pili kwenye Ligi Kuu Bara.

“Sio jambo lakufurahisha kwa washindi wa pili kwenye Ligi Kuu Bara kuishia hatua ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwangu naona haikustahili kuwa hivyo. Kwa upande wako unaweza kuchagua lakusema labda wamezingua, tumechoka, bahati mbaya ama tupotezee.”

Ukiweka kando Azam FC kufungashiwa virago kwenye anga la kimataifa, Coastal Union ya Tanga ilifungashiwa virago na Bravos kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo ni mchezo wa ugenini walifungwa mabao yote katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ilikuwa 0-0.