>

SIMBA KUCHUANA NA AL AHLI TRIPOLI KWENYE HATUA YA KWANZA YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Simba Sc itachuana na Al Ahli Tripoli kwenye hatua ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya miamba hiyo ya Libya kufuzu kwenda hatua hiyo kufuatia ushindi wa jumla wa 5-1 dhidi ya Uhamiaji Fc ya Zanzibar kwenye mchezo wa hatua ya awali.

FT: Al Ahli Tripoli 🇱🇾 3-1 🇹🇿 Uhamiaji Fc (Agg. 5-1)

Mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Simba Sc dhidi ya Al Ahli Tripoli atajikatia tiketi ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika 2024/25.