>

ISHU YA YANGA KUTOA MILIONI 216 KISA OKRA YAMUIBUA JEMBE

ANAANDIKA Jembe kuhusu ishu ya Yanga na Okra Magic.

BAADA ya taarifa kueleza kuwa Yanga wanapaswa kumlipa mchezaji wao wa zamani Okra Magic kiasi cha milioni 216, mwandishi wa Habari za Michezo Tanzania Saleh Jembe ameweka wazi kuwa haifurahishi Yanga kuingia kwenye madeni yasiyo ya lazima kisa usajili wa furahisha genge.

Jembe ameanza namna hii: “Lazima umeisikia taarifa ya kuwa Shirikisho la Soka la Kimataifa( Fifa) limeitaka Klabu ya Yanga kuilipa Klabu ya Bechem United ya Ghana kiasi cha dola za Kimarekani 80,000 sawa na Tsh Milioni 216 ndani ya siku 45 kuanzia sasa ikiwa ni pesa ya malipo yaliyosalia katika uhamisho wa Augustine Okrah kutoka Bechem United kwenda Yanga.

“Kwangu naona hii si sawa Yanga kuendelea kuingia kwenye madeni kupitia wachezaji wa furahisha genge. Najua itakuwa vigumu watu kuelewa kwa kuwa Yanga sasa wanashinda na wako vizuri lakini madeni kama haya na yale ya akina Bigirimana Yanabaki kwenye klabu na yangeweza kuepeukika.

“Ukiangalia usajili wao inakuwa si kukosea lakini ni kama siasa hivi au kutaka kuonyeshana hivi.
Najua taarifa inasema Yanga wanapaswa kuwa wamekubali au kupinga mpaka ifikapo tarehe 3 Septemba 2024 vinginevyo baada ya tarehe hiyo itachukuliwa kuwa wamekubali.

“Kuliko kufika huku haya yanaepukika. Okrah kweli…anyway…kuna haja ya kuzipunguzia mzigo wa madeni klabu zetu  kwa kuongeza umakini kwenye usajili na kuufanya usajili uwe kwa manufaa ya klabu.”

Ikumbukwe kwamba Okra aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba akakutana na Thank You alirejea kwa mara nyingine Bongo kwenye dirisha dogo msimu wa 2023/24 alitambulishwa kwenye Mapinduzi Cup hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25 baada ya kukutana na Thank You.