HUSSEN Massanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa watakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.
Timu hiyo imeweka kambi Dar na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Massanza amesema kuwa wanatambua umuhimu uliopo kwenye ligi hivyo wanafanya kazi kuwa imara kwenye mechi za ushindani ambazo watacheza.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar hivyo kwa sasa tunafanya maandalizi kuelekea mchezo wetu ujao wa ligi na ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri.
“Mchezo wa kwanza tumepata pointi tatu dhidi ya Ken Gold hivyo tunahitaji kufanya vizuri kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Kagera Sugar, tupo tayari na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”
Agosti 24 2024 Singida Black Stars inatarajiwa kushuka Uwanja wa Kaitaba itakuwa saa 1:00 usiku.