>

MERIDIANBET YAFIKA KIGAMBONI SIKU YA UTU DUNIANI

Meridianbet wamesambaza Utu mitaa ya Kigamboni katika siku ya Utu duniani baada ya kufika eneo hilo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa familia duni.

Mara kwa mara mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamekua wakijitahidi kurudisha kwenye jamii yao haswa zile zenye uhitaji kwelikweli, Ndicho walichokifanya leo baada ya kufika kwenye familia zenye uhitaji na kugawa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kama Sukari, Mafuta, Unga, Mchele, na Sabuni.

Meridianbet wameyafanya hayo katika kuuadhimisha siku ya Utu duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 19, Hivo wao wamehakikisha wanarejesha kwenye jamii ambazo zina uhitaji ili kwenda sambamba na wiki hii ya Utu duniani.

 

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

 

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Igram aliongoza zoezi hilo na kufanikiwa kuzungumza machache “Kama inavyofahamika leo tunaadhimisha siku ya Utu duniani na sisi tumeamua kuuonesha Utu wetu kwenu na ndio maana tumefika hapa leo kujumuika na nyie kwa kutoa mahitaji haya muhimu kwenu”

 

Aidha familia ambazo zimeweza kupokea msaada leo kutoka kwa Meridianbet hazikuacha kutoa shukrani kwa mabingwa hao wa michezo ya  kubashiri na kusema makampuni, taasisi zingine zinapaswa kufanya kama ambavyo wamefanya Meridianbet kwa kuzikumbuka jamii zenye uhitaji.