NYOTA wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ikiwa ni Aziz Ki, Clatous Chama, Kibabage wamepewa kazi nzito ya kufanya kwenye anga la kimataifa kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki Agosti 24 2024 na mashabiki kazi yao ni kuvunja rekodi kwa kujitokeza Uwanja wa Mkapa kuwashangilia wachezaji watakapovaana na Vital’O ya Burundi mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.