>

AZAM FC WAIPIGIA HESABU APR KIMATAIFA

YUSUPH Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wana uwezo wakupata matokeo ugenini dhidi ya APR katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na uimara wa kikosi Chao.

Katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-0 APR.

Ni dakika ya 55 nyota Jhonier Blanco alipachika bao pekee la ushindi akifungua code kwa mguu wa kulia likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Penalti hiyo ilisababishwa na kiungo Feisal Salum ambaye alichezewa faulo akiwa ndanj ya 18.
Kocha Dabo ameweka wazi kuwa APR sio timu ndogo wanaiheshimu kutokana na walivyopambana mbele yao.

“Tulikuwa na muda wakupata matokeo na niliwaambia wachezaji kuwa ukipata nafasi ya kufunga fanya hivyo ikishindikana itakuwa ni muda wakutoa pasi kwa mwingine.

“APR ni timu ngumu kufungika kwani haijafungwa mabao mengi kutokana na uimara wao katika ulinzi bado tuna nafasi yakupata matokeo ugenini kwa kuwa tuna kikosi imara na cha ushindani.”

Kocha Mkuu wa APR ya Rwanda Darko Novic amesema kuwa ni mchezo uliokuwa wazi na walihitaji kupata ushindi mwisho wakapoteza kwa kukosa nafasi ambazo walitengeneza.

“Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani lakini tulikosa nafasi ambazo tulizipata mwisho tukafungwa kwa penalti ambayo imewapa ushindi hivyo tutafanya maandalizi mchezo ujao.”