>

MWAMUZI KUTOKA ESWATINI NDIYE ATAKAYESIMAMIA MCHEZO WA HATUA YA AWALI KATI YA AZAM NA APR

Mwamuzi kutoka Eswatini, Thulani Sabelo Sibandze ndiye atakayesimamia mchezo wa hatua ya awali kati ya Azam FC na APR FC katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Mtanange huo utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi Agosti 18 majira ya saa kumi na mbili kamili za jioni.

APR FC ndio Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Rwanda msimu uliopita ambapo pia walikipiga na Simba SC kwenye “Simba Day” katika kupima kikosi kuelekea Ligi Kuu na Mashindano ya Kimataifa.