>

MERIDIANBET WAHAKIKISHE MBEZI MPIRA UNACHEZWA

Kampuni ya Meridianbet leo ilikua ina kazi moja tu ya kuhakikisha kua mpira wa miguu unachezwa bila tabu ya aina yeyote ndani ya eneo la Mbezi jijini Dar-es-salaam kwa kugawa vifaa vya michezo.

Huu umekua utamaduni wa wababe hao wa michezo ya kubashiri kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yao haswa kwa wale wenye uhitaji, Ambapo leo ilikua zamu ya Mbezi haswa kwa vijana wanaopenda mpira wa miguu ambapo Meridianbet imegawa mipira kadhaa.

Kama ambavyo inatambulika serikali inajitahidi kuhakikisha inainua sekta ya michezo kwakua ni moja ya sekta ambazo zimekua zikitoa ajira kwa vijana, Hivo Meridianbet wameamua kuinga mkono serikali kwa kuhakikisha nao watoa ushirikiano katika kukuza michezo nchini na ndio sababu wametoa msaada wa mipira leo katika eneo la Mbezi.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Ingram alikua mbele kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na kusema “ Nina furaha kubwa kuwepo mahali hapa leo na kama mnavyojua michezo imekua moja ya sekta muhimu kwa vijana kupata ajira siku hizi, Hivo sisi tumeamua kuhakikisha tunawashika mkono vijana wa eneo hili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika suala zima la michezo haswa mpira wa miguu”

 

Aidha Diwani wa Jimbo la Mbezi ya Juu Mheshimiwa Anna Lukindo alikuwepo katika zoezi hilo bila kusita alizungumza machache “ Kiukweli niwashukuru sana Meridianbet kwa kufika hapa leo na kuweza kutoa msaada wa vifaa vya michezo ambavyo vitawasaidia vijana wetu wanaopenda michezo kufikia malengo yao, Lakini pia nipende kutoa rai kwa makampuni mengine wanaweza kuiga haya mazuri ambayo yanafanywa na Meridianbet kuhakikisha wanaisaidia jamii yao”