UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa kwa msimu wa 2024/25 wataanza kazi kwa nguvu na sio kinyonge kwenye mechi tano za mwanzo ndani ya Ligi Kuu Bara.
Ipo wazi kwamba msimu wa 2023/24 haukuwa bora kwa timu hiyo iliyogotea nafasi ya 11 baada ya mechi 30 ilikomba pointi 33 ilishinda mechi 8 iliambulia kichapo kwenye mechi 13 huku sare ikiwa katika mechi 9 za ligi.
Ni Agosti 18 Singida Fountain Gate itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Namungo kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Issa Liponda wengi wanapenda kumuita Mbuzi ameweka wazi kuwa wanakwenda kufanya kweli kwenye mchezo wao wa kwanza wakiwa na hesabu za kufanya kazi kubwa ya kusaka pointi kwenye mechi tano za mwanzo.
“Tumeona ratiba imetoka na hilo tunalitambua kwa kuwa maandalizi tulianza kufanya awali na muda wa kutoa burudani umefika. Kwenye mechi zetu tano za mwanzo msako wa pointi 15 tunamalengo yakuvuna kuanzia pointi 7 ikiwa hamnahamna inaweza kugotea kwenye pointi 6.
“Wachezaji, benchi la ufundi lipo kamili kwa mechi zetu zote za ushindani mashabiki wawe pamoja nasi kwenye kila mchezo iwe nyumbani ama ugenini, kama mbwaimbwai.”