PAZIA LA LIGI KUU BARA LINAFUNGULIWA

BAADA ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 kukamilika kwa timu zote ndani ya Bongo sasa pazia la Ligi Kuu Bara linakwenda kufunguliwa ikianza mzunguko wa kwanza ndani ya ligi.

Ipo wazi kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga ilitwaa taj hilo likiwa ni la 30. Baada ya kucheza mechi 30 ni pointi 80 zilikuwa kibindoni itaperusha bendera kwenye anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Agosti 17 itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Vital’ O ya Burundi hatua ya awali wakiwa ugenini.

 Ni Pamba Jiji hawa kutoka jiji lenye mawe kila kona watafungua pazia itakuwa Agosti 16 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Agosti 17 itakuwa Mashujaa v Dodoma Jiji Uwanja wa Lake Tanganyika na Namungo wataikaribisha Fountain Gate Uwanja wa Majaliwa.

Simba itatumia Uwanja wa KMC itamenyana na Tabora United, Agosti 18  na Singida Black Stars kete yao ya kwanza watakuwa ugenini dhidi ya Ken Gold itakuwa ni Agosti 18 2024.