MWAMBA KUTOKA MWANZA MWANZA AMEACHIA ZAWADI HII

LEGEND kwenye muziki Bongo Fareed Kubanda ambaye ni mzawa kutoka Mwanza ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Simba.

Kazi hiyo ameiachia muda mfupi ikiwa ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani Agosti 13 ambapo kwenye nyimbo yake ya Agosti 13 akiwa na Salam Jay na Juma Nature alibainisha kuwa alizaliwa katika Hospital ya Bugando, Mwanza.

Nyota huyo mkali wa michano ya Hip Hop amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu na kazi yake ya kuelimisha jamii ikizidi kupasua anga kitaifa na kimataifa.

Miongoni mwa mastaa ambao wanakubali kazi ya mwamba huyo ni pamoja na Stamina ambaye ni kutoka Morogoro.

Yupo a Mex Cortez pamoja na Lord Eyez Fid Q, Ngosha amesema kuwa sio kila anachokilenga huwa ana nia ya kukipata.

Maisha mema Ngosha, Mungu azidi kukulinda kila wakati.