WIKI YA MOTO, NGAO YA JAMII HII HAPA

WIKI hii ni yamoto kutokana na matukio yake kuwa bamba kwa bamba kutokana na kila timu kuwa kazini ikiwa ni kuelekea katika msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ipo wazi kuwa kutakuwa na Big Day ya ni Agosti 10 2024 Uwanja wa Liti ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa kuelekea kwenye tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na Pamba Day itafanyika Mwanza Agosti 10 2024 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tayari kuna matamasha ambayo yamegota mwisho ikiwa ni Simba Day Agosti 3 2024 na Wik ya Wananchi ilikuwa ni Agosti 4 2024 yote haya mawil yalifanyika Uwanja wa Mkapa.

Kazi inaendelea ambapo wiki nyingine imeanza mwendelezo wa matukio upo palepale ambapo kunatarajiwa kuchezwa Ngao ya Jamii kwa timu za nne bora kushuka uwanjani.

Ipo namna hii 8/8 2024 itakuwa nusu fainali kati ya Azam FC v Coastal Union, Uwanja wa New Amaan, Zanzibar saa 10:00 jioni Yanga v Simba, Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku. Agosti 11 itakuwa mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Uwanja wa Mkapa saa 9:00 alasiri.

Agosti 11 2024 itakuwa fainali kwa mshindi wa nusu fainali ile ya Uwanja wa Amaan na Uwanja wa Mkapa.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 taji la Ngao ya Jamii lilibebwa na Simba kwa ushindi wa penalti dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.