JEMBE: KIBU HAKUSTAHILI KUCHEZA, MASHABIKI WALISTAHILI KUMZOMEA

LEGEND kwenye masuala ya uandishi wa Habari za Michezo kitaifa na Kimataifa Saleh Ally wengi wanapenda kumuita Jembe ameweka wazi kuwa Kibu Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba hakupaswa kucheza mchezo wa Simba Day.

Ipo wazi kwamba Agosti 3 2024 ilikuwa kilele cha Simba Day Uwanja wa Mkapa ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 APR na miongoni mwa wachezaji waliocheza ni Kibu, Mohamed Hussen, Ally Salim, Edwin Balua.

Jembe amesema:”Kibu hakustahili kucheza ile mechi kwa kuwa amewakosea sana Simba na kuzomewa na mashabiki alistahili kwani kitendo alichofanya ilikuwa ni cha hovyo, alikuwa anatambua ana mkataba na fedha za Simba amechukua lakini hakujiunga na timu kambini.

“Inaelezwa kuwa kocha alikuwa anahitaji kuona Kibu anacheza lakini tumeona namna ilivyokuwa hakuwa fiti kabisa na alicheza hovyo hivyo hakupaswa kabisa kucheza mchezo ule.”

Kibu hakuwa na Simba kambini nchini Misri na alirejea timu ikiwa Bongo alifanya mazoezi na timu siku moja kabla ya mchezo wa Simba Day uliochezwa Agosti 3 2024 na Simba kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR mabao yakifungwa na Deborah Fernandes na Edwin Balua.