MCHAMBUZI wa soka Bongo, Mzee wa Jambia ameweka wazi kuwa msimu bora wa Fei Toto umepewa tuzo ya MVP wa CRDB huku MVP wa NBC Aziz Ki naye akiwa anastahili kile ambacho amekifanya. Mzee wa Jambia amebainisha kuwa alikuwa anatamani kuona kwamba Feisal anapata tuzo ya MVP wa NBC msimu wa 2023/24.